
Hadithi ya 13
Bahari Inafunguka
Kutoka 14:5–31
Watu wa Mungu walipotoka Misri, Farao alibadili nia, akatuma jeshi lake na magari ya vita kuwafuata. Waisraeli walikuwa wamepiga kambi kando ya bahari, na walipoliona jeshi likija waliogopa sana. Musa akawaambia, 'Msiogope. Simameni imara mwone jinsi Bwana atakavyowaokoa.' Nguzo ya wingu ilihamia nyuma yao, ikawatenganisha na jeshi.
Musa aliunyoosha mkono wake juu ya bahari. Usiku mzima upepo mkali ulivuma, na maji yakagawanyika, pakawa na nchi kavu katikati na ukuta wa maji kila upande. Watu walivuka salama. Kisha maji yakarudi mahali pake, na jeshi halikuweza kuwafuata tena. Watu wakamcha Bwana, wakamwamini yeye na Musa mtumishi wake.
Watoto wanajifunza: Hata tunapoogopa na kuona hakuna njia, Mungu anaweza kufungua njia, nasi tunaweza kumtumaini.