Rudi mwanzo
Akaunti
Futa akaunti yako
Unaweza kufuta akaunti yako ya Biblia Yangu wakati wowote, hapa au ndani ya programu (Eneo la mzazi → Futa akaunti yangu).
Kitakachofutwa
Watoto uliowaongeza, mahali walipofikia kwenye hadithi, hadithi wanazozipenda, simu zilizoingia kwenye akaunti, maendeleo ya kusoma kwenye tovuti, na usajili wa habari kwa namba hii.
Kitakachobaki bila jina wala namba yako
Kumbukumbu za mauzo (tarehe, bidhaa na kiasi) zinazotakiwa kisheria. Haki za kusoma vitabu ulivyonunua zinasitishwa.