Biblia Yangu
Rudi mwanzo

Faragha

Sera ya faragha

Biblia Yangu ni kwa ajili ya familia. Tunakusanya kidogo iwezekanavyo, hatuonyeshi matangazo, na hatuuzi taarifa za mtu yeyote.

Imesasishwa: 19 Septemba 2026

Sisi ni nani

Biblia Yangu ni chapa ya Protend, kampuni iliyosajiliwa Tanzania.

Programu ya Biblia Yangu

Programu inatumika bila akaunti. Mzazi akiingia, tunahifadhi namba yake ya simu, na aina ya simu na toleo la programu kwa ajili ya usalama wa kuingia. Mzazi anaweza kuongeza watoto kwa jina la utani, picha kutoka kwenye orodha yetu na kundi la umri tu — hakuna jina kamili, tarehe ya kuzaliwa wala picha halisi. Tunahifadhi mahali kila mtoto alipofikia, hadithi anazozipenda na mahali alipoishia kusikiliza, ili ziwe sawa kwenye simu zote za familia. Programu haiombi mahali ulipo, anwani za simu, kamera wala kipaza sauti, na haina matangazo. Pia inatuma takwimu za matumizi bila majina (kwa mfano hadithi ngapi zimesomwa) ili tuiboreshe; mzazi anaweza kuzizima kwenye Eneo la mzazi.

Tovuti

Unapoagiza kitabu tunahitaji jina, namba ya simu na anwani ya kupeleka. Ukijiunga na orodha ya habari tunahifadhi barua pepe yako (na namba ukiiweka) na ulichochagua kupokea. Tovuti inatumia Google Analytics kujua kurasa zinazotembelewa.

Tunazitumia kwa nini

Kutuma namba za uthibitisho kwa SMS, kukuletea oda zako, kukupa vitabu ulivyonunua, kusawazisha maendeleo ya watoto kati ya simu zako, na kukutumia habari ulizoomba tu.

Tunashirikiana na nani

Watoa huduma wanaotusaidia tu: Beem Africa (SMS), Amazon SES (barua pepe), Cloudflare (kuhifadhi picha na sauti za vitabu), watoa huduma wa seva zetu, na Google Analytics kwa tovuti. Hatuuzi wala kukodisha taarifa za mtu yeyote.

Watoto

Watoto hawafungui akaunti. Mzazi ndiye anayeongeza profaili zao na anaweza kuzibadilisha au kuzifuta wakati wowote. Eneo la mzazi kwenye programu limefungwa kwa swali la hesabu.

Tunahifadhi kwa muda gani

Taarifa za akaunti zinabaki hadi utakapofuta akaunti. Kumbukumbu za mauzo tunazihifadhi kwa muda unaotakiwa na sheria ya kodi, bila jina wala namba yako baada ya kufuta akaunti.

Haki zako

Unaweza kuomba kuona, kusahihisha au kufuta taarifa zako. Unaweza kufuta akaunti yako mwenyewe kwenye programu au kwenye ukurasa wa Futa akaunti.

Futa akaunti yako